Habari

Majaliwa atoa maagizo kuhusu Uviko-19

Waziri wa Mkuu, Kassim Majaliwa, amewaagiza wakuu wa mikoa kutoa elimu na uhamasishaji juu ya  umuhimu wa kuchanja chanjo ya uviko-19.

Waziri Mkuu, Majaliwa

Mh. Majaliwa amesema hayo leo Jijini Dodoma, Oktoba 4 2021, kwenye ufunguzi wa Kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

Amesema suala la chanjo sio lazima lakini ni muhimu kwa afya kwaasababu linasaidia kuongeza virutubisho mwilini na iwapo mtu atapata hawezi kuwa sawa na mtu ambaye hajachanjwa kabisa katika kukabiliana na virusi hivyo.

“Tunalo zoezi la uchanjaji. Namshukuru Mungu tumefikia asilimia 80 na kitu huko, tumebaki na chanjo chache sana kwenye mikoa hiyo. Kila mmoja awahi huko na kama kuna mahitaji tutaleta nyingine malengo ni afya,” amesema.

Majaliwa amesema mpaka sasa zipo dalili nzuri kwenye kukabiliana na virusi hivyo, ingawa ugonjwa  bado upo na watu wanapaswa kuendelea kujikinga kwa kufuata kanuni zote zinazotolewa na Wataalamu wa  Afya, ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi yanayostahimilika na miili.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents