BurudaniHabari

Majizzo ampiga Diamond na kitu kizito, afungua studio mpya ya kisasa

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia studio mpya ya EFM ambayo imetambulishwa leo na Mkurugenzi wa media hiyo Francis Cizza alimaarufu kama Majjizo.

Studio hiyo ni ya kisasa kabisa na vifaa vyake ni vya kisasa kabisa na inawezekana ikawa studio ya kwanza ya kisasa Afrika Mashariki nzima kwa namna ilivyo na vifaa vyake vilivyo.

Majjizo ameeleza dhumuni lake la kuanzisha studio hiyo ya kisasa kabisa ambayo ilihudhuriwa na Mtangaza ngumi wa Tanzania Salm Kikeke.

Katika ule mchuano wake an Diamond bwana Majizzo alimaarufu Profesa au Mzee wa Telescope hapa amempiga Diamond maana walianzisha batle ya uwekezaji kwenye media zao.

Kwa namna alivyofanya uboreshaji kwenye upande wa vifaa hapa tunasema Majizzo ameondoka na alama zote Tatu.

Studio hiyo ina kila kitu cha kisasa kabisa huenda tukaona Diamond naye akaja na uwekezaji wa aina yake kwenye media yake na watu wanachotaka ni upinzani wa kibiashara na sio kingine.

@el_mando_tz anasema Upinzani wa Kibiashara sio mbaya tena Diamond na yeye anatakiwa kuja na kitu kipya maana huo upinzani walianzisha wao na unajenga tasnia haubomoi.

Anaongeza tena upinzani wao unatakiwa usapotiwe na kila mtu kwani unaboresha tasnia, wanapoongeza upinzani wao wa kibiashara tasinia nayo inakua.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents