Habari

Makadinali 20 wateuliwa kupata mrithi wa Papa Francis

Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis mwishoni mwa wiki akiwa mjini Vatican amewatawaza makadinali 20 wakiongezwa kwenye kundi la wale wanaohitajika kuchagua mrithi wake  baada ya kifo au kujiuzulu.

Miongoni mwa waliotawazwa wakati wa hafla hiyo kwenye kanisa ya St Peter Basillica, 16 miongoni mwao walikuwa na umri wa chini ya miaka 80, ikiwa na maana kwamba wanaweza kushiriki katika kumchagua Papa mpya. Wakati akichagua makadinali hao,

Papa Francis alionyesha kuzingatia wale pia kutoka jamii zilizotengwa. Miongoni mwa waliochaguliwa ni askofu Peter Ebere Okapaleke mwenye umri wa miaka 59 kutoka Nigeria.

Askofu mkuu Hyderabad Anthony Poola mwenye umri wa miaka 60 ni wa kwanza kuchaguliwa kutoka kwenye jamii yenye hadhi ya chini zaidi nchini India.

Pamoja na makadinali hao 20 wapya, Papa Francis mwenye umri wa miaka 85 sasa ameteua jumla ya makundi manane ya makadinali 83 kutoka jumla ya 132 wenye umri wa kujiunga kwenye kundi la kuchagua mkuu mpya wa kanisa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents