BurudaniMakala

Makala: Kauli ya Marioo haitoshi kusema Diamond ni muongo, aitolee ufafanuzi kulinda mahusiano

Kauli ya Marioo haitoshi kusema Diamond ni muongo, aitolee ufafanuzi kulinda mahusiano

Moja kati vitu muhimu kwa kampuni, taasisi au brand ni mahusiano mazuri na watu unaofanya nao kazi au jamii kwa ujumla. Mahusiano ya Umma tunaweza kusema ni mchakato wa mawasiliano ya kimkakati ambao huunda uhisiano wa faida kati ya mashirika na hadhira yao.

Gumzo mtandaoni kwa sasa ni msanii @marioo_tz kukataa kwamba hakumuomba @diamondplatnumz kujiunga na WCB.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa WCB wiki hii kueleza jinsi alivyodai kuombwa na msanii huyo kujiunga na lebo hiyo ambayo ina mafanikio makubwa Tanzania.

Kauli ya Marioo kumtakaa Diamond imeripotiwa na mitandao mingi baada ya hit maker huyo Mi Amor ku-comment kwenye ujumbe wa @mwijaku uliotaka msanii huyo kueleza kwanini aliomba kujiunga na WCB.

MARIOO ALIMAANISHA KUMKATAA DIAMOND?

Kutokana na sintofahamu hiyo, Marioo aliandika “Hahahahah mkubwa kateleza mfupa hauna ulimi” kauli ambayo bado haitoi majibu ya moja kwa moja kwamba amemkataa Diamond.

Katika hatua nyingine huwenda Marioo alimua kumtakaa Diamond ili kulinda brand yake, baada ya kuona tayari ameweza kufanya makubwa katika muziki wake kwa kutegemea mashibiki wake.

KAULI YA DIAMOND HAIKUWA NA UBAYA KWA MARIOO.

Kauli ya Diamond akihojiwa na Wasafi alieleza jinsi alivyotembelewa na Marioo nyumbani kwake, bila shaka ni nafasi ambayo wasanii wengi wanaitaka kwa kuwa rais huyo wa WCB ni mmoja kati ya wasanii wenye mafanikio kwenye kila nyanja.

“Marioo alikuja nyumbani alitaka nimsaini,” alisema Diamond

Aliongeza “Sikiliza nilichomwambia, Marioo mimi nikikutazama naona unafanya vizuri, nahisi kukusaini sikutendei haki,”

Kwa mujibu wa kauli hii ya Diamond inaonyesha hakuwa na lengo baya, bali alitaka kuonyesha ni jinsi gani Marioo alivyomkubwa na fursa zinazomzunguka.

Maoni ya mashabiki yanasema Diamond alidanganya, kwa kauli ya Marioo ambayo haiko wazi sana.

Kwa mantiki hiyo, Marioo ana sababu yakunyoosha maelezo kwa kauli ya Diamond ambayo ilikuwa wazi, Vinginevyo kwa mengi wataamini ni kweli aliomba kusainiwa ila amekataa ili kufuta aibu ya mashabiki huku mahusiano yake na WCB yakiharibika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents