Makamba asitisha ukusanyaji wa Mabilioni kuanzia kesho

Waziri wa Nishati, Januar Makamba ametangaza kuwa kuanzia kesho Oktoba 06, Taasisi kadhaa chini ya Wizara yake zitaacha kukusanya kodi ili kuwapa unafuu watumiaji wa mafuta nchini.

Kauli ya Waziri Makamba imekuja muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuelekeza kupunguzwa kwa Tozo kwenye Mafuta.

Taarifa ya Rais juu ya kupunguzwa kwa tozo

Katika taarifa ya Waziri amesema “kuanzia kesho, taasisi kadhaa zitaacha kukusanya jumla ya bilioni 101 ili kutoa nafuu kwa wananchi.

Tumepokea maelekezo ya Mhe Rais na leo tuta-‘gazette’ upunguzaji wa tozo nane za Serikali zinazochangia kwenye bei za mafuta ili kupunguza makali ya ongezeko la bei za mafuta duniani,” Waziri Makamba.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button