Makala

Makampuni ya simu za mkononi yanavyosaidia ukuaji wa biashara ndogondogo na za kati (SMEs)

Tanzania imeshuhudia ukuaji mkubwa wa kuridhisha wa biashara ndogo na za kati (SMEs).

 

Kwa mujibu wa Chemba ya Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), biashara ndogo na za kati zinajumuisha asilimia 95 ya biashara zote nchini Tanzania, na zinachangia asilimia 35 ya Pato la Taifa (GDP).

Pamoja na kuwa kichocheo kikubwa cha kusukuma mbele maendeleo ya kiuchumi, SMEs inajimuisha mashirika kutoka sekta mbalimbali za uchumi kama vile kilimo, usafirishaji na biashara.

Kwa pamoja mashirika/kampuni hizi zimesaidia kuleta mabadiliko chanya katika uchumi wa Tanzania kwa kuzalisha ajira, kukuza ubunifu, kutoa huduma na bidhaa kwa watu wa kipato cha chini, pamoja na kuchukua nafasi kubwa katika kuwajumuisha wanawake, na vijana katika uchumi.

Ni wazi kuwa SMEs itaisaidia Tanzania kwa kiwango kikubwa kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Hata hivyo, licha ya mafanikio hayo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii, bado SMEs zinakumbana na changamoto mbalimbali katika ukuaji wake.

Miongoni mwa changamoto kubwa zinazozikumba biashara hizi ni pamoja na ugumu wa kupata huduma za kifedha, pamoja na kukosekana kwa huduma ya intaneti iliyo imara yay a kuaminiwa.

Lakini, sekta binafsi bado imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa ufumbuzi wa changamoto hizo unapatikana.

Kampuni ya Tigo Tanzania ni moja ya mifano ambayo imekuwa ikijishughulisha kuwakikisha inaboresha mazingira ya kibiashara ili kuhakikisha kuwa zinazidi kukua kila iitwapo leo.

Hivi karibuni kampuni hiyo ilitangaza kuzinduliwa kwa huduma ya intaneti ya ofisi, huduma ambayo imeletwa madhubuti kuhakikisha inaboresha upatikanaji wa inatenti katika SMEs.

Huduma hiyo inatoa uwezo wa vifaa hadi 32 kwa wakati mmoja ambapo vifaa hivyo vitaweza kupata intaneti yenye kasi ya 4G+, na kuweza kutumia programu mbalimbali kupitia Microsoft 365.

Mbali na hilo, wamiliki wa biashara ndogo na za kati wanaweza kupata faida nyingine kwa kuwa mawakala wa huduma ya Tigo-Pesa.

Kwa kufanya hivyo zitakuwa zinarahisisha ufanyaji wa biashara kwa kuungana na makampuni zaidi ya 70,000 ambayo yanakubali malipo kwa njia ya simu, pamoja na kulipa ankara mbalimbali kupitia huduma ya Tigo Pesa Wallet.

Kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali ambazo zinakumba biashara hizi, Tigo inasaidia kuongeza uzalishaji wan chi, pamoja na kutoa fursa za kiuchumi kwa idadi kubwa sana ya Watanzania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents