Makamu mwenyekiti Yanga, Fredrick Mwakalebela afungiwa miaka mitano

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia miaka mitano Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga , Fredrick Mwakalebela kujishughulisha na mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa makosa ya kimaadili.

Mwakalebela pia ametozwa faini ya Sh 5,000,000 baada ya kutiwa hatiani kwa kutoa maneno ya uchochezi kwa nia ya kuchochea washabiki, wanachama na wapenzi wa Yanga dhidi ya vyombo vinavyosimamia mpira wa miguu nchini.

Uamuzi huo wa Kamati umetolewa kwa kuzingatia kifungu cha 73(4) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.

Related Articles

Back to top button