Habari

Makonda aripoti kwa Chongolo na kupewa baraka zote

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komredi Daniel Godfrey Chongolo amesema CCM iko salama na imara katika kusimamia misingi, shabaha na malengo yake, ikiwemo kuendelea kuwa daraja la kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.

Amesema kuwa hali hiyo inatokana na jinsi ambavyo CCM kinaendelea kuwatumikia wananchi kwa kuzisimamia Serikali zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan a Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dokta Hussein Ali Mwinyi, ambazo zimeendelea kutafsiri maelekezo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025, kwa vitendo.

Nougu Chongolo amesema hayo Alhamis, Oktoba 26, 2023, alipokutana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Ndugu Paul Christian Makonda na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdallah Hamid, walipofika ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba, jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya kuonana naye, kujitambulisha na kuanza kazi, baada ya kukabidhiwa ofisi zao rasmi na watangulizi wao.

 

Chongolo aliwaelekeza Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Paul Makonda na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Rabia Abdallah Hamid, kuanza majukumu yao, wakitambua imani kubwa waliyopewa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Nougu Dokta Samia Suluhu Hassan, kutumikia Chama kupitia nafasi hizo walizoteuliwa.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Chongolo amesema kuwa nafasi hizo mbili, Idara ya Itikadi na Uenezi na Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, ni mojawapo ya maeneo ya kimkakati ya CCM, hivyo wanapaswa kujua kuteuliwa kwao ni sehemu va kuongeza chachu na kasi ya idara hizo kutekeleza malengo yaliyokusudiwa na CCM, katika kutumikia wananchi na kuzisimamia Serikali zote mbili za CCM.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents