Fahamu

Mali za jambazi maarufu wa Marekani Al Capone zauzwa kwa $3m (+ Video)

Uuzaji wa mali za jambazi maarufu wa Marekani Al Capone umekusanya jumla ya dola milioni tatu za kimarekani (£ 2.2m) kwenye mnada uliofanyika mwishoni mwa wiki huko California.

Baadhi ya vitu 174 – pamoja na silaha za moto na picha za kibinafsi pamoja na vito na samani- zimeonyeshwa.

Hafla hiyo, inayoitwa Karne ya Umaarufu: Mali ya Al Capone, ilifanyika katika kilabu cha kibinafsi na ilivutia wazabuni karibu 1,000.

Bidhaa maarufu zaidi ilikuwa bunduki inayopendwa na Capone, ambayo iliuzwa kwa $ 860,000.

Bunduki ya Al Capon

Bunduki hii inaaminika ilkuwa bei ya juu zaidi ya silaha ya karne ya 20 iliyouzwa kwenye mnada, kulingana na Chicago Tribune.

Al Capone alikuwa mhalifu mkubwa Chicago aliyejulikana kama Adui Namba moja wa Umma kwa utawala wake mfupi kama kiongozi wa uhalifu miaka ya 1920.

silaha
Image caption: Bunduki na vyombo vya glasi ambavyo vilikuwa vya jambazi huyo na mtoto wake Sonny pia viliuzwa

Mali ya Al Capone ilisalia katika milki ya familia yake kwa karibu miaka 75 baada ya kifo chake mnamo 1947.

Kulikuwa pia na picha za kuuza, zilizoonyeshwa hapa kabla ya mnada
Image caption: Kulikuwa pia na picha za kuuza, zilizoonyeshwa hapa kabla ya mnada

Diane Capone – mmoja wa wajukuu watatu wa Al Capone walionusurika, ambao wanaishi California – alisema uamuzi wa kuuza vitu hivyo ulitokana na yeye na dada zake kuzeeka, kulingana na taarifa za shirika la habari la Reuters.

Diane Capone - mmoja wa wajukuu watatu wa Al Capone
Image caption: Diane Capone – mmoja wa wajukuu watatu wa Al Capone.Bofya hapa chini kutazama.https://www.instagram.com/p/CU97KGCDBCA/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents