FahamuHabari

Mali za mwanamke tajiri Afrika, zawekewa kizuizini Angola

Mahakama ya Juu ya Angola imeamuru kuwekewa”kizuizi” kwa mali zenye thamani ya karibu dola bilioni 1 zinazomilikiwa na Isabel dos Santos, binti wa rais wa zamani wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, shirika la habari la Lusa la Ureno lilisema Jumanne.

Hati ya mahakama iliyonukuliwa na Lusa, ya Desemba 19, ilisema mamlaka ina ushahidi wa madai ya ubadhirifu na utakatishaji fedha haramu na ikaamuru kukamatwa kwa fedha za dos Santos katika “taasisi zote za benki”.

Ukamataji huo pia unajumuisha hisa zote za dos Santos katika kampuni ya Angola ya Embalvidro, pamoja na 100% ya hisa katika kampuni ya mawasiliano ya simu ya Unitel T+ ya Cape Verde na Unitel STP huko Sao Tome e Principe, kulingana na Lusa.

Jumla ya 70% ya hisa zake katika MStar na Upstar Comunicacoes za Msumbiji zinapaswa kukamatwa pia, Lusa ilisema.

Dos Santos amekabiliwa na tuhuma za ufisadi kwa miaka. Mnamo mwaka wa 2019, Mahakama ya Juu ya Angola iliamuru kukamatwa kwa mali yake kwa madai ya kusimamia fedha za serikali kwa makampuni ambayo alikuwa na hisa wakati wa urais wa baba yake, ikiwa ni pamoja na kampuni kubwa ya mafuta ya Sonangol.

Baba yke Dos Santos, Jose Eduardo dos Santos, alifariki Julai. Alitawala Angola kwa takriban miongo minne hadi 2017.

Msemaji wa dos Santos hakujibu mara moja ombi la maoni.

Mara kwa mara amekanusha makosa yoyote na aliiambia CNN Ureno mwezi Novemba kwamba mahakama nchini Angola “haziko huru” na kwamba majaji huko “walitumika kutimiza ajenda ya kisiasa”.

Agizo hilo linakuja baada ya shirika la polisi duniani Interpol kutoa notisi nyekundu kwa dos Santos mwezi uliopita, na kuzitaka mamlaka za kimataifa kumtafuta na kumkamata kwa muda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents