
Mikel Arteta amejifunza mengi sana alipokuwa chini ya Kocha Pep Guardiola pale Manchester City kabla ya kupata kibarua cha kuinoa Arsenal.
Msimu wa 2022-23 umekuwa wenye mafanikio makubwa sana kwa Arteta akiwaongoza ‘The Gunners’ kuweka heshima wakiongoza msimamo wa Premier League akiwa na point 50 kabla ya kukutana na Guardiola kwenye FA Cup Ijumaa hii.
Guardiola amepuuza kuhusishwa na mafanikio ya kijana wake Mikel Arteta kuwa alijifunza chini yake mpaka leo amekuwa kuwa tishio kwa timu ndogo na kubwa zinazokutana na moto wa Arsenal.
“Ninachokiona Arsenal kinamuhusu Mikel na watu wake,”- Kauli ya Guardiola kabla ya kukutana na mwanafunzi wake usiku wa leo.
Man City vs Arsenal tutegemee matokeo ya namna gani..?
Imeandikwa na @fumo255