Michezo

Man City wachukua ubingwa wa PL kibabe

Manchester City wamefanikiwa kutwaa Ubingwa msimu wa 2021/22 Premier League ukiwa ni wa nne ndani ya misimu mitano.
Ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa mwisho wa msimu huu umetosha kuwatangaza mabingwa vijana hao wa Guardiola huku wakipishana alama moja tu mshindani wake Liverpool.

Hili linakuwa taji la 11 chini ya Pep Guardiola tangu kujiunga na City mwaka 2016.

Katika mechi 38, Man City imeshinda 29, sare sita (6) huku kikosi chake kikifunga jumla ya magoli 99.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents