Man United milango ipo wazi kuhusu Sancho – Dortmund 

Wakala Mino Raiola amekana tetesi kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland,20. (Goal)

Mtendaji Mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amesisitiza kuwa klabu yake inamipango na Haaland msimu ujao. (Dazn via Mirror)

Hatahivyo, Bosi huyo anasema klabu hiyo itasikiliza ofa kwa ajili ya winga wa England Jadon Sancho. (Manchester Evening News)

Winga wa England Jadon Sancho

Winga wa England Jadon Sancho

Kocha Pep Guardiola amesema Manchester City wanaweza kuamua kutumia zaidi ya pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji mmoja siku za usoni, lakini ameendela kuwa na kigugumizi juu ya tetesi kuhusu klabu yake kuhusishwa na Haaland. (Sky Sports)

 

Barcelona itaendelea na mipango yake ya kumnada mchezaji huyo wa Norway baada ya kukutana na wawakilishi wake wiki iliyopita, lakini vyanzo katika klabu hiyo wanasema kuwa itakuwa”vigumu sana” kutekeleza azma yao. (ESPN)

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amevunja ukimya ukimya kuhusu tetesi za uhamisho zinazomuhusisha mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah,28, kuhamia Bernabeu. (Liverpool Echo)Mohamed Salah

Je mshambuliaji wa Misri na Liverpool Mohamed Salah atahamia Real Madrid?

Villarreal wana matumaini ya kumsajili mlinzi Juan Foyth,23, wa Tottenham msimu huu kwa mkataba wa kudumu kwa kiasi cha chini ya ada ya pauni milioni 13.Kwa sasa mchezaji huyo anacheza kwa mkopo katika klabu hiyo.(Football Insider)

Related Articles

Back to top button