HabariMichezo

Manara amuita Feisal msaliti na mhujumu mkubwa wa Yanga

Kupitia Instagram yake Manara ameandika kuwa “Ni aibu kubwa kwa Nchi ni fadhaa na kulikosea Taifa hili, Kwa mara nyingine tena Fesal Salum anashiriki kuihujumu Yanga Waziwazi bila haya.

Tupo karibu kabisa na finali kubwa mbele yetu,Rais Wa Nchi yupo busy mara kwa mara kuhamasisha watanzania, Bunge kupitia Waziri Mkuu wanahamasisha, Wakuu wa mikoa ndio kama mnavyosikia.

Kisha anatokea Binadamu anaepotoshwa na Watu wale wale kila tunapokaribia mechi kubwa kutuletea mjadala wa jambo lake binafsi lisilokuwa na chembe ya maslahi ya Taifa kutuletea choko choko.

Hiv hii sio hujuma ya kusudi kwetu na kwa nchi? Mawakili wake,Mameneja wake na hata Radio zinazopush agenda yake kipindi hiki tukisema wanatuhujumu kusudi tutakuwa tunakosea?

Kwanza anachangisha nn wakati majuzi tu kaleta Milioni Mia ya kuvunja mkataba? Kwa nn asichukue ile Vits Ya Dalali wake akauza ili aende CAS?

Fesal unaendelea kutengeneza ufa ndani ya mioyo ya wengi, Yanga hii unayotafuta huruma mitandaoni ndio iliyokulea na kukupa jina unalosafiria nalo hv sasa,Yanga hii hii ndio ilipkufanya uwe na hilo jina ambalo hao wanaokudanganya leo walikujulia hapa.

Mbaya zaid Mchambuzi mpumbav yule yule toka Radio ile ile yupo front kuendelea kukupotosha,Taifa linasulubiwa Kwa sababu yako Fei, Nchi ipo ktk vita ya ubingwa,ww unashiriki vita yako ya huruma za kinafik.

Unasema eti mama yako alitukanwa, yy na Yanga nani kamtusi mwenzie? Kutwambia ulikuwa unakula Ugali na Sukari sio matusi na dhihaka kwetu,

Ni kweli mara nyingi umekuwa unatufanyia hv kila tunapokaribia mechi kubwa ,lakini kwa mechi hii nathubutu kumwambia wazi wazi ww ni Mhujumu unaetumika bila kujijua,Ww ni Msaliti,,Ww sio Muungwana hata chembe, unaihujumu Yanga na unawahujumu Wachezaji wenzio mlioishi nao

Why usisubiri mechi iishe? Why iwe leo? Na kwa nn kila mechi yetu kubwa unarudia drama zako?

Tushinde tushindwe hupati hata medali moja, mjinga sana ww Mtoto, unafanya hvyo kwa maslahi gani? Yanga imekukosea nn cha Ziada hadi uwe unatufanyia hvyo na huyo Shankupe wako muuza sumu na nywele za maiti?

Umetutafuta mara nyingi lakini hii ni too much, hujali kabisa kuhusu heshma ya nchi yako kisha eti unataja Team za Taifa! Zipi hzo wakati ww unahujumu maslahi ya Taifa kusudi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents