HabariMichezo

Manchester United yatoa Tamko kuhusu Cristiano Ronaldo

Klabu ya Manchester United imetoa taarifa kuhusiana na mahojiano yaliyofanywa na nyota wao Cristiano Ronaldo na mwandashi wa habari hali iliyopelekea kuzua gumzo kubwa katika ulimwengu wa soka.

Manchester United kupitia website yao wametoa taarifa ifuatayo ”Manchester United asubuhi ya leo imeanzisha hatua zinazofaa kujibu mahojiano ya hivi majuzi ya Cristiano Ronaldo kwenye vyombo vya habari.”

”Hatutatoa maoni zaidi hadi mchakato huu ufikie hitimisho lake.” Wamemalizia Manchester United baada ya staa wa timu hiyo kuongea mambo mengi kuhusu klabu hiyo bila kuacha kumzungumzia kocha wake Erik ten Hag akidai kuwa hamuheshimu kwakuwa hata yeye amekosa kupewa heshima.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents