Kupitia kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumza namna Harmonize anavyojuaga kufanya promo za nnyimbo zake na kuzifanya ku-trend kupitia Attention anazozifanya.
Siku ya jana alitangaza kuachia wimbo wake wa BETTER SIDE ambao unnaeleza kuwa yupo tayari kuwa mchepuko kwa mwanamke anayempenda hatojali kuwa mwanamke huyo yupo kwenye mahusiano au laah.
Lengo inawezekana ni kweli Harmonize anataka kuwa mchepuka lakini ukweli ni kwamba Harmonize anatumia fursa kufanya promo za ngoma zake, ngoma hiyo imeachiwa kionjo tu lakini karibia asilimia kubwa ya watu wanaofuatilia muziki wamejua Harmonize kuan wimbo anataka kuuachia.
Baada ya kutangaza vile, Mange Kimambi amemjia juu baada ya kuhisi kuwa Harmonize anamtaka Hamisa Mobetto licha ya kuwa Mobetto yupo kwenye mahusiano yake.
Inawezekana Mange haujui ukweli maana mapenzi ya nguvu sana, mpaka kufika Harmonize kuandika kitu kama kile ujue kuna namna wamefikia na amepata tumaini kuwa inawezekana.
@el_mando_tz anasema kuwa Harmonize ni wale watu ambao wakishikilia jambo lao lazima ahakikishe amelikamisha kwa vyovyote vile, kama kweli Harmonize anamtaka Hamisa usiseme haiwezekani jua lolote linawezekana.