Manuel Locatelli aikwepa Arsenal, aitamani Juve kisa Champions League

Michuano ya Euro 2020  na Copa America imekwisha na sasa dirisha la usajili barani Ulaya ndio linalochukua nafasi baada ya kufunguliwa rasmi, klabu kubwa kubwa zimeingia sokoni kuhakikisha zinasajili wachezaji watakaoweza kuzisaidia timu zao.

Arsenal 'willing to pay £34m for Manuel Locatelli' but ace wants Juve -  Flipboard

Arsenal imetenga kitita cha Euro milioni 40 kwaajili ya kunasa saini ya kiuongo wa klabu ya Sassuolo, Manuel Locatelli.

Hata hivyo, Manuel Locatelli mwenye umri wa miaka 23 anatamani kuendelea kusalia Italia hasa kwenye klabu ya Juventus kutokana na uwezekano wa kushiriki michuano ya UEFA Champions League ukilinganisha na Arsenal.

Manuel Locatelli yupombioni kukutana na waajiri wake Sassuolo, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye michuano ya Euro 2020, ambapo alifunga jumla ya magoli mawili na akiwa sehemu ya kikosi kilichocheza fainali dhidi ya England.

The Gunners wanadai wanahitaji mchezaji ambaye atashawishika kuijiunga na klabu, hata hivyo kutua Juventus kwa kiungo huyo kutategemeana na uwezo wa kifedha wa miamba hiyo ya soka ya Italia.

Related Articles

Back to top button