Habari

Maporomoko ya udongo yauwa 26 India

Vikosi vya uokoaji vimefanikiwa kupata miili ya watu 26 waliofariki kutokana na maporomoko ya udongo yalioharibu kabisaa kituo cha ujenzi wa reli kaskazini mashariki mwa India.

Kazi ya uokoaji inatarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa lakini kuna matumaini hafifu ya kupatikana manusura kati ya watu 37 ambao hawajulikani walipo tangu siku ya Jumatano.

Afisa wa uokoaji, Pankaj Kavidayal, amesema watu 21 kati ya 26 waliothibitishwa kufariki walikuwa wanajeshi waliopelekwa eneo hilo kutoa ulinzi kwa maafisa wa reli kutokana na miongo kadhaa ya uasi wa makundi ya kikabila yanayotaka kujitenga katika eneo hilo.

Tangu Mei 17 mwaka huu, takriban watu 200 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko katika majimbo ya Assam, Manipur, Tripura na Sikkim nchini India, huku wengine 42 wakifariki nchini Bangladesh. Wanasayansi wanasema mabadiliko ya hali ya hewa ndio chanzo cha hali hiyo isiyokuwa ya kawaida.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents