BurudaniHabari

Mapungufu show ya Diamond Ruangwa, Rayvanny amemkalisha??

Kupitia kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia kuhusu show ambazo zilifanyika kwenye Tamasha la Wasafi Festival ambalo lilifanyika siku ya Jumamosi mkoani Lindi katika wilaya ya Ruangwa.

Tamasha hilo linajumuisha wasanii wengin sana Tanzania ambao ni karibia wote ni A List ya wasanii nchini.

Katika Tamasha hilo watu wanaendelea kujionea ubunifu kwa wasanii wetu ili kuboresha kazi zao wanazozifanya, wasanii kama Diamond, Rayvanny na Whozu wanaongoza kufanya mambo mbalimbali jukwaani kuonyesha namna gani wanajiongeza.

@el_mando_tz anasema kuwa Rayvanny na Diamond ndio walitikisa kwenye ubunifu zaidi na hasa Rayvanny aliwavutia wengi kwa namna alivyofanya tukio lililoendana na uhalisi wa maisha ya watu wengi.

Kwa upande wa Diamond alifanya ubunifu mzuri lakini kwa asilimia kubwa ubunifu wake hakuendanna na maudhui ya nyimbo zake, @el_mando_tz anasema sio kwamba alikosea ila kuna sehemu yannahitajika marekebisho tu.

ametoa mfano wimbo wa My Baby, Zuwena na Yatapita hata Enjoy huwezi kutumbuiza nyimbo za mapenzi mbele yake kuna majeneza na mafuvu, kuna namna uhalisia haukuwepo.

Watu wa ubunifu wa Diamond wanatakiwa kurekebisha baadhi ya mambo ili show za msanii mkubwa kama Diamond ziendana na uhalisi, kiukweli kwenye suala la ubunifu baadhi ya wasanii wanafanya vizuri sana.

@el_mando_tz anasema kuwa katika show zijazo anaamini kuwa maboresho yatafanyiwa kazi ili kuendelea kukuza Tamasha pendwa la Wasfi Festival.

Unakubaliana na @el_mando_tz ??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents