Kupitia kwenye kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz leo ameizungumzia ngoma mpya ya Baba Levo na Diamond Amen na kusema kuwa ni wimbo mzuri sana wenye ujumbe mzuri sana pia Ilaa…
Kuna vitu Baba Levo anetakiwa kuviongeza na vingine kuvipunguza ili kuweza kuleta uhalisia wa ujumbe alioamua kuuwasilisha kwa jamii yake.
Baadhi ya vitu ambavyo @el_mando_tz anahisi vingekuwepo ni pamoja na kuvaa mavazi yanayoendana na ujumbe unaowasilishwa lakini pia Mavideo Vixen pia kuna namna wangetakiwa ku-dress ili waendana na ujumbe pia ikiwemo namna ya kucheza na nguo walizovaa.
Pia kuna baadhi ya scenes wanamuomba Mungu lakini vifua wazi pia, sio kitu kibaya ila pia sio kitu kizuri.