Mapya kuhusu Mikopo Kidigitali

Tanzania leo imezindua rasmi huduma ya eMkopo, mkopo wa kidigitali uliobuniwa mahsusi kwa ajili ya watumishi wa umma, kupitia ushirikiano rasmi na Mfumo wa Serikali wa Watumishi Portal (https://ess.utumishi.go.tz).
Huduma hii inawawezesha watumishi wa umma nchini kuomba na kupata mkopo wa hadi TZS milioni 200, kwa kipindi cha kurejesha cha hadi miezi 108 (sawa na miaka 9), kwa njia rahisi na ya kidigitali bila kulazimika kutembelea matawi ya benki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Emmanuel Mahondanga, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi
“Uzinduzi wa eMkopo unaashiria hatua kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha zinazozingatia mahitaji ya sasa. Kwa kuunganishwa na mfumo wa serikali wa Watumishi Portal, tunarahisisha mchakato mzima wa upatikanaji wa mikopo kwa watumishi wa umma – kwa njia ya haraka, salama na rafiki kwa mtumiaji. Hii ni sehemu ya dhamira yetu ya kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kuchochea ustawi wa wateja wetu.”
Naye Priscus Kavishe, Meneja Mwandamizi wa Mauzo na Upatikanaji Wateja aliongeza:
“eMkopo ni matokeo ya ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi, unaolenga kuwahudumia kwa ufanisi watumishi wa umma. Kupitia Watumishi Portal – ambayo ni jukwaa rasmi la Serikali – mteja anaweza kuomba mkopo wa hadi TZS milioni 200 kwa njia ya kidigitali, na kuurejesha kidogo kidogo kwa kipindi cha hadi miaka 9. Tunahakikisha huduma hii inawafikia kwa urahisi na kwa masharti rafiki.”
Ili kuomba mkopo huu, mtumishi wa umma anapaswa kuingia kwenye Watumishi Portal kupitia kiungo: