Habari

Marekani ina Imani ya kudhibiti Vitisho vya Uchaguzi ujao November.

Mamlaka nchini Marekani zinasema wana imani kuwa wataweza kukabiliana na vitisho vyoyote vya usalama kuelekea uchaguzi wa rais mwezi Novemba.

Huko Alexandria, Virginia, Mwandishi wa VOA, Veronica Balderas Iglesias alihudhuria mafunzo ya maafisa wa uchaguzi, moja ya hatua kadhaa za kuhakikisha upigaji kura huru, wa haki na wazi.

Mwezi uliopita, maafisa wa juu wa Marekani waliliambia Bunge kuwa uchaguzi wa Rais wa Marekani utakuwa wa haki na salama, shukran kwa kuimarisha ulinzi na kuongeza ushirikiano kati ya serikali kuu, mamlaka za majimbo na serikali za wilaya.

Jen Easterly, Mkuruguenzi wa Shirika la Usalama wa Mitandao na Miundombinu ya Kiusalama, kaskazini mashariki Washington, amesema: “Kuanzia uhalifu wa mitandao, mpaka vitisho vya kimwili, hatari za uendeshaji, na kutoka kwa ushawishi mbaya wa kigeni. Jombo moja la kuangalia, hapo kuna utofauti katika miundo mbinu ya uchaguzi wetu, kwasababu unashughulikiwa na serikali, na mamlaka 8,800 tofauti kote nchini, kwahiyo utofauti unaipa uthabiti.

FILE - Makao Makuu ya Shirika la Usalama wa Mitandao na Miundombinu ya Kiusalama, kaskazini mashariki Washington.
FILE – Makao Makuu ya Shirika la Usalama wa Mitandao na Miundombinu ya Kiusalama, kaskazini mashariki Washington.

Katika mji wa Alexandria, Virginia, kwa mfano, mashine za kura hazijaunganishwa na nainternet, na hivyo kuufanya utaratibu kuwa salama zaidi dhidi ya majaribio ya udukuzi.

Angie Maniglia-Turner, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Alexandria alisema: “Kwa kuongezea, tunajaribu mashine kabla ya kila uchaguzi kwa kupitia mchakato mrefu wa kina na pia kujaribu utendaji wake kuhakikisha kwamba zimetengenezwa mahsusi kwa kazi hiyo.”

Kuhakikisha mchakato wa wazi, mji unatoa mafunzo kwa mpaka maafisa wa uchaguzi 500 kwa ajili ya chaguzi za awali na uchaguzi mkuu mwezi Novemba. Wanajifunza kuhusu nini kinahitajika katika upigaji kura pamoja na jinsi ya mashine za kupigia kura zinavyoweza kufanya kazi na kuidhinisha matokeo ya eneo la uchaguzi.

Julie Podolsky, Afisa Uchaguzi amesema: “Watu wangapi wamefika. Wangapi, unajua, kura zao zimeingia kwenye mashine, na hili linatokea kutwa nzima na watu tofauti wanafanya hivyo. Tunabadili nafasi zao. Kwahiyo hakuna njia utakuwa na timu nzima ya watu kufanya uratibu ili kuanya jambo lolote lisilo la kawaida.”

Kutokana na mazingira yaliyopo na uwezekano wa vitisho, afisa uchaguzi Marc Dyer na wengine pia wanajifunza mbinu za kupunguza kasi.

Marc Dyer, Afisa Uchaguzi anaeleza: “Mara moja moja sana kutakuwa na mtu ambaye ana vurugu au amekuwa na siku mbaya, mpiga kura, lakini mara nyingi hali inakuwa nzuri.”

Wachambuzi waliohojiwa na VOA pia walitarajia hilo, kwa jumla, uchaguzi ujao wa rais utakwenda vizuri.

Anton Dahbura, Taasisi ya Habari na Usalama, Johns Hopkins alisema: “Kuna macho mengi sana yanayoangalia mfumo wa uchaguzi wetu, na maadui kwa kweli hawalipendi hilo. Wanakuwa kama maleno rahisi, mambo ambayo watu kwa kweli hawayaangalii. Na hivyo, nahisi kwamba kwa sababu hizo, kwa kweli hakutakuwa na tukio la usalama wa aina yoyote katika uchaguzi wa 2024.”

Lakini kuna aina nyingine ya kitisho ambacho wapiga kura ni vyema wafahamu, watetezi wa uchaguzi wanasema.

Susannah Goodman, Mkurugenzi, Common Cause Election Security anaeleza: “Kuna habari potofu na habari potofu zinazungumziwa kuhusu mifumo ya upigaji kura na jinsi mambo yanavyofanya kazi kudumaza imani katika mchakato wetu wa demokrasia. Nadhani hilo kwa hakika linatia wasi wasi mkubwa.”

Wapiga kura wa Marekani wanashawishiwa kuwa katika tahadhari; wafanyakazi wa kujitolea wa uchaguzi wa wasimamizi wenyewe; na kuwafikia mamlaka kama wana maswali jinsi mchakato wa uchaguzi unavyofanya kazi.

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

CHANZO: VOA SWAHILI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents