Habari
Marekani inatarajia kusaini mkataba wa madini na Ukraine

Trump amesema pia kwamba juhudi za kufikia makubaliano ya amani katika mzozo kati ya Urusi na Ukraine zimefikia katika hatua nzuri baada ya kufanya mazungumzo wiki hii na marais Vladimir Putin wa Urusi na Volodymyr Zelensky wa Ukraine.
Hayo yanajiri wakati hapo jana viongozi wa mataifa ya Ulaya wamekubaliana kuongeza matumizi yao katika sekta ya Ulinzi kwa kutenga euro bilioni 800 ifikapo mwaka 2030.
Pia wameafikiana kuongeza msaada wa kijeshi kwa Ukraine ili iendelee kukabiliana na uvamizi wa Urusi.