
Marekani, Israel na Misri zimekubaliana kusitisha mapigano kusini mwa Gaza ili kuwiana na kufunguliwa tena kwa kivuko cha mpaka cha Rafah, vyanzo viwili vya usalama vya Misri vimeliambia shirika la habari la Reuters.
Reuters ilisema usitishaji wa mapigano ungeanza saa 06:00 GMT – sasa – huku kukiwa na ripoti za vyombo vya habari kwamba kivuko kinachodhibitiwa na Misri kitafunguliwa tena kwa wakati mmoja.
Vyanzo viwili vya usalama vya Misri vimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba usitishaji vita kusini mwa Gaza utaendelea kwa saa kadhaa – ingawa hawajaweka wazi kuhusu muda halisi.
Pia walisema Israel, Misri na Marekani zimekubali Rafah “itafunguliwa hadi 14:00 GMT” Jumatatu kama ufunguzi wa kwanza wa siku moja.
Walipoulizwa kuthibitishwa, jeshi la Israel na Ubalozi wa Marekani nchini Israel hawakuwa na maoni ya mara moja, Reuters inaongeza.
Bado hatujaweza kuthibitisha ikiwa kivuko kimefunguliwa.
Hamas inasema haina taarifa kuhusu usitishaji vita – ripoti
Mkuu wa ofisi ya vyombo vya habari vya Hamas anasema hawana taarifa kuhusu makubaliano ya kusitisha vita kwa sababu za kibinadamu yaliyokubaliwa kusini mwa Gaza, kulingana na Reuters.
Salama Marouf ameliambia shirika hilo la habari kwamba hawajapata uthibitisho wowote kutoka upande wa Misri kuhusu nia ya kufungua kivuko cha Rafah kati ya Gaza na Misri.
Kivuko cha Rafah kinaweza kufunguliwa kwa muda mfupi pekee – Marekani
Marekani inatarajia kuwa hali katika kivuko cha Rafah kati ya Misri na Gaza “itabaki kuwa shwari na haitabiriki” huku kukiwa na ripoti kwamba kitafunguliwa saa 09:00 kwa saa za huko – karibu sasa.
Ikitoa ushauri kwa Wamarekani huko Gaza, wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema haijafahamika iwapo watu wataruhusiwa au kwa muda gani kupita kivuko cha kusini.
“Ikiwa utatathmini kuwa ni salama, unaweza kutaka kusogea karibu na kivuko cha mpaka cha Rafah – kunaweza kuwa na taarifa ndogo sana kama kivuko kikifunguliwa na kinaweza kufunguliwa kwa muda mfupi,” inasema.
Maafisa wanashughulikia “chaguo zinazowezekana za kuondoka” kwa Wamarekani huko Gaza.
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Israel-Gaza