Habari

Marekani, Urusi kubadilishana wafungwa

Urusi imesema leo kuwa inafanya mazungumzo na Marekani juu ya uwezekano wa awamu nyingine ya kubadilishana wafungwa lakini hadi sasa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa.

Hayo yameelezwa kupitia taarifa ya msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi ambayo imesema Moscow ina matumaini mazungumzo yanayoendelea yatazingatia maslahi ya pande zote.

Marekani ilitangaza hapo jana kuwa imewasilisha pendekezo kwa Moscow la kuachiwa huru wamarekani wawili wanaoshikiliwa nchini Urusi ikiwemo mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu Brittney Griner.

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken alisema anapanga kufanya mazungumzo na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov mnamo siku zinazokuja kujadili suala hilo.

Hata hivyo Blinken amekataa kuthibitisha fununu kwamba Marekani inapanga kutekeleza ubadilishanaji wafungwa kwa kumwachia huru mlanguzi wa silaha wa Urusi Viktor Bout anayetumikia kifungo cha miaka 25 nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents