Habari

Marekani, Urusi zakubaliana kupunguza mvutano Ukraine

Marekani na Urusi zimekubaliana kushirikiana katika juhudi za kuupunguza mvutano kuhusu Ukraine.

 


Marekani imeahidi kujibu kwa maandishi matakwa ya usalama ya Urusi wiki ijayo na kutoufuta mkutano wa rais.

Wakati hofu ikiongezeka kwamba Urusi inaweza ikaivamia kijeshi Ukraine, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amerudia kutoa onyo la kulipiza kisasi kwa kuchukua hatua kali wakati alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov mjini Geneva, Uswisi.

Baada ya mkutano huo, wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilisema Lavrov alionya kuhusu madhara makubwa zaidi iwapo Marekani itaendelea kuyapuuza matakwa ya usalama ya Urusi.

Blinken amesema hakuna hatua kubwa iliyopigwa katika mazungumzo hayo, lakini anaamini kuwa pande hizo mbili “ziko kwenye njia nzuri na iliyo wazi” kuelewa wasiwasi na msimamo wa kila mmoja kwenye mzozo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents