Habari

Marekani yaitaka Rwanda kuacha kuwasaidia M23

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken amemwambia Rais wa Rwanda Paul Kagame kuacha kutoa msaada kwa kundi la waasi la M23 linalopigana na serikali ya Kinshasa, mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema kwamba, Blinken amefanya mazungumzo ya simu na Rais wa Rwanda Paul Kagame na kuzungumzia umuhimu wa kuwepo amani na utulivu mashariki mwa DRC.

Blinken amesema kwamba Marekani inaunga mkono juhudi za amani zinazofanywa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na mpatanishi wa umoja wa Afrika, ambaye ni rais wa Angola Joao Lourenco.

Rwanda imekuwa ikikana kila mara shutuma kwamba inaunga mkono waasi wa M23, lakini taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price, inasema kwamba Blinken amesisitiza kwamba “msaada wowote kwa makundi ya waasi yanayopigana Congo lazima ukome mara moja.

Rais Paul Kagame amekuwa akisema kwamba Rwanda haihusiki na vita vinavyoendelea nchini Congo, na kwamba kinachofanyika nchini humo ni waasi wanaotaka makubaliano waliofikiwa na serikali ya Kinshasa kutekelezwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents