Marekani yalaani hatua ya Nigeria kuifungia Twitter

Marekani imelaaani vikali hatua ya serikali ya Nigeria kufungia mtandao wa Twitter nchini humo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Ned Price amesema hatua hiyo ya Nigeria si tu inakiuka uhuru wa demokrasia lakini pia inakandamiza uhuru wa kujieleza.

Wiki iliyopita Nigeria iliamua kufungia mtandao huo kutoa huduma nchini humo baada ya mtandao huo kufuta moja ya chapisho la rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari kwa madai lilikuwa ni la uchochezi.

Pamoja na kufungiwa kwa mtandao huo, ili kuendelea kutumia mtandao huo, baadhi ya wanigeria wanatumia VPN

Serikali yenyewe ya Nigeria ilisema kufungiwa kwa mtandao huo hakuna uhusiano wowote na kuondolewa ama kufutwa kwa chapisho la Rais Buhari.

Chapisho hilo la Buhari lilieleza kuwashughulia watu wote hasa vijana ambao wamekuwa wakuharibu miundo mbinu ya serikali.

Related Articles

Back to top button