Marekani yatoa tahadhari Usalama Msumbiji
Marekani imetoa tahadhari ya usalama kwa raia wake nchini Msumbiji hasa katika mji mkuu wa Maputo.
Hatua hiyo ni kufuatia kuongezeka kwa maandamano katika maeneo mbalimbali mjini Maputo, zikiwemo barabara zinazoelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo, na katika miji mingi kote Msumbiji.
Ubalozi wa Marekani mjini Maputo umewataka raia wake kufahamu hali hiyo ya dharura.
Hapo jana Tume ya uchaguzi nchini humo ilitangaza kwamba chama tawala cha Msumbiji, Frelimo, kimeshinda uchaguzi uliogubikwa na mgawanyiko, ghasia, na hivyo kurefusha muda wa miaka 49 madarakani wa chama hicho katika taifa hilo la kusini mwa Afrika, Tume ya Uchaguzi imetangaza.
Daniel Chapo, mgombea urais wa Frelimo ambaye hajulikani kwa kiasi fulani ambaye ameonekana kuwa mwanamageuzi, atachukua nafasi ya Filipe Nyusi, ambaye amehudumu kwa mihula miwili.
Akiwa na umri wa miaka 47, Chapo, ambaye alipata 71% ya kura, atakuwa rais wa kwanza kuzaliwa baada ya uhuru wa Msumbiji mwaka 1975.
Mpinzani wake wa karibu, Venancio Mondlane alipata 20% ya kura.
Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ghasia zilizuka katika miji kadhaa ya nchi hiyo huku kukiwa na ripo za maafa na watu wengi kujeruhiwa.