Burudani

Mariah Carey afiwa na mama na dada siku moja

Mamake Mariah Carey Patricia na dada yake Alison walifariki siku moja mwishoni mwa juma, mwimbaji huyo wa Marekani amesema katika taarifa yake.

“Moyo wangu umeumia sana kwa kumpoteza mama yangu wikendi hii iliyopita,” Carey alisema Jumatatu.

Dada wa Mariah Carey

“Cha kusikitisha zaidi, dada yangu pia alipoteza maisha siku hiyo hiyo.”

Mwimbaji huyo aliyeshinda tuzo ya Grammy alisema alijihisi mbarikiwa kwa kutumia muda wake akiwa na mama yake wiki moja kabla ya kifo chake na kuomba kupewa faragha. Hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu sababu za vifo vyao.

Katika kumbukumbu, mnamo mwaka 2020, Mariah Carey, alieleza kwa kina uhusiano wake wenye utata na mama yake, akisema ulikuwa umemsababishia “maumivu na mawazo mengi “.

Patricia, 87, alikuwa mwimbaji wa zamani wa opera na kocha wa sauti mwenye asili ya Ireland na Marekani. Carey alizungumzia upendo mwingi aliokuwa nao kwa mama yake, na kuandika: “Kwa Pat, mama yangu, ambaye, katika yote hayo, naamini kwa kweli alifanya yote aliyoweza.

Mariah Carey akiwa na Mama yake

Nitakupenda kwa namna niwezavyo, siku zote.” Katika mahojiano na Gayle King mnamo 2022, mwimbaji huyo alisema “bila shaka” aliathiriwa na ukosoaji kutoka kwa mama yake alipokuwa akikua. Aliongeza kwamba alikuwa akimsifu mamake kila mara kwa kumtambulisha kwa muziki

Mariah Carey

Uhusiano wa Carey na dada yake mkubwa Alison, 63, pia haukuwa mzuri vile.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents