Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariMahojiano

Marioo ameisusa album yake?? unahisi kwanini haifanyii tour mikoani??

Kupitia kwenye kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumza namna ambavyo msanii wa muziki wa Bongo Fleva Marioo alivyoisusa Album yake ya THE KID YOU KNOW.

@el_mando_tz anasema kuwa ilipaswa msanii Marioo kufanya tour ya Albm yake na sio kuisusa kama alivyoifaya kwa sasa kwanni inaonyesha kabisa hanna mpango wa kuifayia hata tour ya angalau mikoni mitano Tanzania.

Anaongeza kuwa mbali ya kuwa ataitangaza album yake lakini pia ni njia nzuri ya yeye kutengeneza kipato chake kwani muda ndio huu wa sasa akiwa anafanya vizuri kwenye soko la muziki.

Marioo ni mmoja ya wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa nchini lakini kuna sehemu ukienda mikoani ndani ndani kuna watu huenda wanasikiliza nyimbo za Marioo lakini sura yake huenda hawaijui.

Tour ndio njia pekee ambayo wasanii wote duniani huitumia kwa lengo la kutangaza kazi zao na hata wao kujitangaza pia, wasanii wote duniani wakitoa album zao huwa wanafanya tour

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents