AfyaHabari

Marufuku kutoka nje kwa muda wa wiki tatu- Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa amri ya watu kutotoka nje ya Wilaya mbili ambazo mlipuko wa virusi vya Ebola ulianzia, kwa muda wa siku 21.

Museveni amesema kwamba serikali inafanikiwa kudhibithi maambukizi ya ebola nchini humo. Amri hiyo itatekelezwa kadi Disemba tarehe 17.

Awali kulikuwa na amri kama hiyo ya siku 21 kuanzia Oct 15, na ilimalizika Nov 5.

Yoweri Museveni ameongeza  kwamba hatua hiyo imechukuliwa ili kuhakikisha kwamba mafanikio ambayo yamepatikana kufikia sasa katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola, yanaendelea na kuhakikisha kwamba hakuna kabisa maambukizi ya virusi hivyo nchini humo katika muda wa siku chache.

Serikali imesema kwamba hakuna maambukizi mapya yameripotiwa katika wilaya hizo mbili

Watu 141 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola nchini Uganda. 55 wamefariki tangu Septemba 20 mlipuko uliporipotiwa.

Hakuna chanjo dhidi ya virusi vya Ebola aina ya Sudan vinavyoripotiwa Uganda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents