Habari

Marufuku ya kusafiri haitokizuia kirusi cha Omicron kusambaa – WHO yaonya

Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO limezionya nchi kutoweka marufuku ya jumla ya kusafiri kutokana na kirusi kipya cha Omicron. Wanasayansi wanajaribu kubaini ni kiasi gani cha kinga ambacho chanjo za sasa zinaweza kutoa.

Serikali mbalimbali na wanasayansi wanajaribu kubaini ni kiasi gani cha kinga ambacho chanjo za sasa zinaweza kutoa dhidi ya kirusi hicho.

WHO imezitaka nchi kutumia mbinu ya ushahidi na athari zilizopo wakati wa kutangaza hatua zozote za kusafiri, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuwachunguza au kuwaweka karantini abiria wa kimataifa.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema anafahamu kuna wasiwasi kuhusu Omicron, lakini marufuku ya jumla ya kusafiri haitokizuia kirusi hicho kusambaa.

Olaf ScholzOlaf Scholz anataka chanjo ya lazima itolewe kwa umma

Kampuni ya BioNTech imeelezea matumaini kuwa chanjo inayotengeneza kwa ushirikiano na Pfizer inaweza ikatoa kinga imara dhidi ya Omicron. Visa vya kirusi hicho kipya vimesambaa, huku kisa cha kwanza kikiripotiwa Amerika Kusini nchini Brazil.

Nchini Ujerumani kansela mtarajiwa Olaf Scholz amesema ataunga mkono pendekezo la kutoa chanjo ya lazima kwa kila mtu mwaka ujao, lakini wabunge watakuwa huru kupiga kura kulingana na hisia zao kuhusu suala hilo.

Wanasiasa Ujerumani sasa wanataka kuwekwe masharti makali zaidi ya kudhibiti virusi vya corona baada ya kiwango cha maambukizi cha siku saba nchini humu kuvunja rekodi.

Msemaji wa masuala ya afya wa chama cha Kijani Janosch Dahmen ameliambia shirika la habari la dpa kwamba kuna haja ya uchumi kufungwa kwa muda katika baadhi ya majimbo ili kulivunja wimbi la nne la maambukizi.

Tamko lake linakuja wakati ambapo kumekuwa na maandamano kaskazini mashariki mwa Ujerumani huku waandamanaji wakipinga vikwazo vipya vinavyowekwa kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.

Wakati huo huo Mahakama Kuu ya Kikatiba nchini Ujerumani imetoa hukumu yake ya kwanza ambapo imesema uamuzi wa kuzuia shughuli za maisha na uhuru wa watu katika kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona ulikuwa halali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents