FahamuHabari

Mashabiki wa Arsenal Uganda washauriwa na Polisi

Msemaji wa Polisi nchini Uganda, Fred Enanga, amewashauri mashabiki wa timu ya Arsenal waliokuwa wamekamatwa baada ya kuandamana kwa gwaride la kushangilia timu yao kwamba ikitokea timu yao imepata ushindi tena dhidi ya Man United watoe taarifa mapema kwa jeshi hilo ili wasisumbuliwe.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Fred Enanga, akiwa na mashabiki wa Arsenal

Januari 22, 2023, mashabiki wa timu hiyo mjini Jinja nchini Uganda, walikamatwa na polisi baada ya kuanzisha gwaride la kushangilia ushindi wa mabao walioupata dhidi ya Manchester United.

“Nimewashauri mashabiki wa Arsenal mjini Jinja kuwashirikisha polisi mapema katika kusherehekea kwao endapo watapata ushindi dhidi ya Manchester United ili kuepukana na usumbufu wa aina yoyote kwenye harakati zao za ushangiliaji,” amesema Enanga.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents