HabariMichezo

Mashabiki wa Arsenal wakamatwa

Polisi nchini Uganda imewakamata jumla ya mashabiki 20 wa klabu ya Arsenal waliokuwa wakisherehekea ushindi wa magoli 3-2 uliyopata timu hiyo dhidi ya Manchester United.

Mashabiki hao 20 walikamatwa kwenye mji wa Jinja kutokana na kusababisha kero kwa kufanya Gwaride mitaani wakisherehekea ushindi huo jana siku ya Jumapili.

Baker Kasule, ni mmoja wa mashabiki wa Arsenal waliokamatwa na polisi amesema kuwa askari wa doria walishuka kwenye gari na kuwataka kuingia.  “Sijui tumefanya nini, tulikjuwa tukisherehekea ushindi wetu dhidi ya Manchester United.”

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button