Michezo

Mashabiki wa Mbeya uso kwa uso na Taifa Stars

Bia ya Serengeti Lager leo imewakutanisha uso kwa uso baadhiya wachezaji wa Taifa Stars na mashabiki katika hafla ya chakula cha jioni iliyofanyika jijini Mbeya ikiwa ni muendelezowa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’

Kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars inalenga kuwapa nafasimashabiki wa Taifa Stars kukutana na nyota wanaowapendakatika baa zao na pia watapata fursa ya kuwauliza maswalikuhusu maisha yao nje ya soka pamoja kupiga nao picha zaukumbusho. Kampeni hiyo ya nchi nzima itadumu kwa miezimitatu.

Akiongea wakati wa hafla hiyo, meneja masoko wa kanda za juukusinini wa SBL Denis Tairo alisema bai ya Serengeti lager ikiwa kama shabiki mkuu wa Taifa Stars inajivunia kuwaleteamashabiki wa Taifa Stars mkoani Mbeya nyota inaowapenda nakuwapa nafasi kuzungumza nao na hivyo kuwafahamu kwaundani zaidi.

“Shabiki mkuu na mdhamini wa timu yetu ya taifa, Taifa StarsBia ya Serengeti Lager leo amewakutanisha mashabiki wa hapaMbeya uso-kwa-uso na nyota ambao mara nyingi wamekuwawakiwaona uwanjani. Hii ni fursa pekee ya mashabiki kujuamaisha ya nota wao nje ya uwanjani,” alisema

Denis alisema kampeni hiyo ya nchi nzima itahusisha wachezajiwa Taifa Stars ambapo watatembelea mikoa ya Mbeya, Mwanza na Arusha na kukutana na mashabiki wao kupitia matukio kamapati za mwisho wa mwezi ‘Nje ya Dimba na Stars’. Kwenyematukio kama hayo mashabiki wataweza pia kujishindia zawadimbali mbali na ofa za bei yao pendwa ya Serengeti lager.

“Wachezaji watakuwa kwenye baa mbali mbali na wakati watejawetu wa bia ya Serengeti Lager wakiendelea kuburudika na biayao pendwa iliyotengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 naisyoongezwa sukari, watapata nafasi ya kuwauliza maswali, kupiga picha na kupata sahihi zao,” alisema

Aliwataka mashabiki wa Stars kutembelea kurasa za mitandaoya kijamii ya bia ya Serengeti Lager Pamoja na kusikiliza rediokwa ajili ya kujua linin a wapi nyota wa taifa Stars watakuwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents