Mashabiki wa PSG hawataki utani na timu yao, baada ya kuliamsha kwa Messi wakaamua kwenda mpaka nje ya nyumba anayoishi Naymar sehemu inayoitwa Bougival katika jiji la Paris
Walipofika wala hawakutaka kuingia bali walianza kuimba nje ya nyumba hiyo wakimtaka na yeye kuondoka kwenye timu yao.
Neymar yupo nje ya uwanja muda umepita sasa na hiyo ni kutokana na majeraha aliyoyapata uwanjani.
Baada ya kufika nyumbani kwa Neymar inaelezwa kuwa kuna uwezekano mkubwa Neymar hayupo Ufaransa yupo nyumbani kwao Brazil.
Wanaimba ‘NEYMAR OUT’