Mashabiki wa soka waliochanjwa tu watangalia mechi bure Afrika Kusini

Shirikisho la soka nchini Afrika Kusini limesema mwezi ujao litatoa tiketi za bure kwa mashabiki wote wa soka waliopata chanjo ya corona kuingia bure uwanjani kushuhudia mechi za kufuzu kombe la dunia kati ya timu ya taifa hilo Bafana Bafana, na Ethiopia.

Shirikisho hilo limesema , mashabiki waliopata chanjo watapewa kipaumbele katika mechi na matukio mengine ya kiburudani.

Serikali ya Afrika ya kusini imekuwa ikiongeza juhudi katika kuwahamasisha watu kupata chanjo. Ni watu milioni 10 tu ndio wamepata chanjo hiyo mpaka sasa ingawa serikali inahitaji kuwafikia watu 40.

Related Articles

Back to top button