Habari

Masharti dhidi ya Corona yalegezwa China

Miji kote nchini China leo imelegeza zaidi vikwazo vya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona pamoja na sheria za upimaji na karantini kutokana na maandamano ya kitaifa ya kutaka kuondolewa mbali kwa vikwazo hivyo na uhuru mkubwa wa kisiasa.

Vyombo vya usalama nchini China vimeingilia kati kwa haraka kutuliza maandamano hayo na kupeleka maafisa wengi wa usalama katika maeneo hayo huku vikiimarisha udhibiti mtandaoni na ufuatiliaji wa raia.

Miji mingi sasa imeanza kulegeza vizuizi vya corona kama vile kuacha upimaji wa watu wengi kila siku, hatua ya kuchosha chini ya sera kali ya Beijing ya kutokomeza ugonjwa wa Covid 19.

Kanda za video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii hapo jana jioni, zilionesha mamia ya watu wakikabiliana na maafisa wa afya nje ya shule moja huko Yicheng, katika eneo la kati mwa jimbo la Hubei.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents