HabariSiasa

Mashirika ya ndege Nigeria kusitisha safari kuanzia Jumatatu

Muungano wa mashirika ya ndege nchini Nigeria umesema utasimamisha safari zote za ndege kuanzia kesho Jumatatu kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

Muungano huo umesema bei ya mafuta ya ndege imepanda kutoka Naira 190 za Nigeria hadi Naira 700 kwa lita. Muungano huo umesema hakuna shirika lolote la ndege duniani linaloweza kustahamili gharama kubwa ya uendeshaji.

Muungano huo umesema itamlazimu abiria kulipa hadi dola 289, kwa safari ya ndege ya saa moja kiasi ambacho raia wengi wa Nigeria ambao tayari wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha, hawataweza kumudu.

Wizara ya usafiri wa anga imeutolea mwito muungano huo kuzingatia athari za kusitisha safari za ndege kwa Wanigeria na wasafiri wa kimataifa.

Nigeria inazalisha mapipa milioni 1.4 ya mafuta ghafi kwa siku, japo inasafisha kiasi kidogo tu cha mafuta hayo. Nchi hiyo hutegemea mafuta yanayoagizwa kutoka nje na kufanya soko la ndani kutatizika iwapo kutatokea uhaba wa bidhaa hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents