Je wajua Uyoga aina ya Matsutake ndio Uyoga wenye gharama kubwa zaidi duniani ambao nusu kilo huuzwa kwa Dollar 500(sawa na shilingi milioni moja na laki tatu za kitanzania).
Uyoga huu unapatikana zaidi nchi za Japan, Korea, China na hata Marekani, lakini ule unaovunwa eneo la Kyoto nchini Japan ndio unaoheshimiwa na wenye bei kubwa zaidi.
Inaelezwa kuwa Matsutake ya kijapani huthaminiwa kutokana na harufu umbile na ladha yake ilivyo ya tofauti kabisa kwa mujibu wa watumiaji.
Imeandikwa na Mbanga B.