Habari

Matumizi ya silaha za nyuklia yaongezeka kwa dola Bil1.4 

Kampeni ya kimataifa ya kuondoa silaha za nyuklia ICAN, imesema katika ripoti yake mpya mataifa tisa yenye silaha za nyuklia duniani yameendelea kuongeza matumizi yake kwenye silaha hizo kwa dola bilioni 1.4, licha ya janga la corona kulemaza uchumi wa dunia.

Nuclear weapons spending swelled $1.4 bn amid pandemic: report - World -  Dunya News

Ripoti hiyo imesema wakati vitanda vya hospitali vilijaa wagonjwa, madaktari na wauguzi kufanya kazi masaa ya ziada huku vifaa vya msingi vya kitabibu vikikosekana, mataifa tisa yalijikuta yakiwa na zaidi ya dola bilioni 72 kwa ajili ya silaha zao za maangamizi makubwa.

Marekani ilitumia zaidi ya nusu ya kiwango hicho, ikiwa imetumia dola bilioni 37.4, hii ikiwa ni karibu asilimia tano ya matumizi yake ya kijeshi mwaka uliopita.

Kwa mujibu wa makadirio ya ICAN, China inaaminika kutumia karibu dola bilioni 10, na Urusi dola bilioni 8.0. Yakichukuliwa kwa pamoja, ripoti hiyo iligundua kuwa mataifa ya nyuklia ambayo pia yanahusisha Uingereza, Ufaransa, India, Israel, Pakistan na Korea Kaskazini, yalitumia zaidi ya dola 137,000 kila dakika katika mwaka 2020.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents