Habari

Maua Sama ni moto, tuchochee tu kuni tunaona mengi (Video)

Jumatano hii muimbaji @mauasama ameachia video ya wimbo mpya Toto. Ni mmoja kati ya wasanii wa Tanzania waliobarikiwa sana kwa sauti, uandishi, muonekano pamoja na ladha ya utofauti sana kwenye muziki wake.

Huyu ni mmoja kati ya wasanii mwenye namba kubwa ya followers mtandaoni kupitia muziki wake mzuri ambao amekuwa akiufanya bila hata kiki.

Licha ya juhudi zake pamoja na za wadau wa muziki kumfikisha hapo alipo ila bado kuna vitu fulani ana stahili, ni msanii ambaye ukimuangalia unaona ni mkubwa hata kuliko fulani, au ana kila kitu zaidi ya wengi ambao wanapewa fursa kisa kiki, ushkaji na mabusu mtandaoni.

Vijana wanasema keki ya muziki ni kubwa, Je ni wasanii wangapi wa kike wanaweza kula keki hiyo kwa kutumia vijiti kama Wachina?.

Vanessa Mdee aliwahi kulalamika na kutangaza kuacha muziki na sababu zikiwa ni
zile zile, wadau wa muziki kuleta ushkaji kwenye biashara.

Maua Sama ameachia video ya wimbo Moto, ni moto kweli kutokana na uhodari wake wakuwakilisha, ni msanii ambaye kwa sasa anahitaji wafanyabiashara halisi wa muziki na mashabiki ‘royal’ ambao ni wasanii wachache sana wanao na wasanii hao wamefanikiwa.

Kwa upande wa mashabiki, tunakosa sana uhondo na ladha kutoka kwa Maua Sama, ni wamoto sana yaani hajawahi kupoa kabisa wala kutoa boko kwenye ngoma zake, naamini tukichochea kuni zaidi kwa kumsupport, basi moto utawaka na tutapata vingi zaidi.

Wahenga husema “Kinga na kinga ndipo moto huwakapo.”
Maana yake moto huwaka baada ya kijinga kimoja kuunganishwa na kijinga kingine cha moto.

Related Articles

Back to top button