FahamuHabari

Mauzo ya Iphone yadaiwa kushuka Duniani (Video)

Huku biashara ikidorora, Apple imekuwa chini ya shinikizo kuonesha itawapa nini wanunuzi wake kuimarisha wimbi jipya la mauzo ya iPhone.

Siku ya Jumatatu, kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ilizindua – iPhone 16 ambayo ina kitufe cha kamera upande wa nje ya simu.

Kitufe hicho ni kidokezo cha mabadiliko ambayo Apple ilisema kuwa imefanya kwenye simu yake mpya, yenye lengo la kutumia akili mnemba (AI).

Mtendaji mkuu wa Apple Tim Cook alisema hatua hiyo “itaboresha kile ambacho simu ya smartphone inaweza kufanya” lakini kampuni hiyo inakumbana na ushindani mkubwa, kwasababu kampuni zingine tayari zimejumuisha AI kwenye simu zao.

Mauzo ya iPhone – bidhaa muhimu zaidi ya Apple ambayo inachangia karibu nusu ya mauzo yake yote – yamekwama katika miezi ya hivi karibuni.

Yalipungua kwa 1% katika kipindi cha miezi tisa iliyomalizika Juni 29 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Apple ilisema simu yake mpya, ambayo ina betri yenye kudumu kwa muda mrefu, chipu zenye nguvu zaidi na vipengele vya faragha vilivyoimarishwa zaidi, zilikuwa za kwanza kutengenezwa mahsusi kwa ajili ya AI na vinginevyo vipya kwenye simu hiyo, ambavyo vingi vilitangazwa mnamo mwezi Juni.

Imeandikwa na @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents