Technology

Mazingira bora ya uwekezaji ni nguzo ya ukuaji wa sekta ya mawasiliano ya simu

Teknolojia ya dijitali imebadili nchi nyingi barani Afrika.

Programu mpya za simu zimesaidia biashara za kila namna kuibuka na kukua.

Mabadiliko haya yamekuwa na tija kubwa kwenye sekta ya ajira na uzalishaji mali na yameleta ahueni kiuchumi kwa nchi nyingi barani hapa.

Katika nchi yangu za Afrika maendeleo haya ya kidijitali yamewezakana kutokana na uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya mawasiliano pamoja na serikali za nchi husika kuunga mkono juhudi za sekta za sekta binafsi kisera na kimkakati.

Wiki hii kampuni nguli ya teknolojia duniani ya Microsoft imetia tena msisitizo kuhusu umuhimu wa kujenga ujenzi katika teknolojia barani Afrika ili kuhakikisha bara hili linavuna faida za teknolojia siku hadi siku. Mkurugenzi wa Microsoft kwa eneo Mashariki ya Kati na Afrika Ibrahim Youssry, ameweka bayana kwamba kampuni hiyo ni mbia wa kudumu wa bara hili katika kujenga uchumi unaotegemea maarifa, kusaidia mtaala wa elimu unaoendana na mabadiliko ya teknolojia na kujengea uwezo vijana.

Takwimu zinaonyesha kwamba toka mwaka 2017, Microsoft imesaidia vijana zaidi ya milioni barani Afrika kuongeza ujuzi na thamani katika kazi zao na hivyo kuwaweka katika mazingira bora zaidi ya kuweza kuajiriwa.

Mbali na hiyo zaidi ya wajasiriamali 1,500 wanaochipukia Afrika wamewezeshwa na Microsoft kuanzisha na kuendesha biashara zao.

Maendeleo haya pia yanategemea ukweli kwamba ili uchumi uimarike, siku zote serikali na sekta binafsi hufanya kazi pamoja.

Mfano mwezi jana, serikali ya Nigeria na kampuni nyingine kubwa ya teknolojia duniani, IBM wametia saini makubwaliano (MoU) ya kufanya kazi pamoja kupunguza idadi ya watu ambao bado hawafaidi matunda ya kukua kwa huduma za dijitali.

Makubaliano hayo yatasaidia sana raia wa Nigeria hasa wa vijijini.
Nchini Tanzania, karibu miongo miwili sasa kampuni binafsi zimekuwa mstari wa mbele kusaidia maendeleo ya kidijitali.

Sekta ya mawasiliano ya simu imekuwa mstari wa mbele kwenye hili hasa tunapoangalia uwekezaji mkubwa ambao imefanya katika teknolojia.

Takwimu zinaonyesha kuwa sekta hii mpaka sasa imewekeza zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 6.Hiki si kiwango kidogo lakini lazima kuhakikisha uwekezaji unaendelea kuongezeka ili sekta ikue zaidi na faida zake ziongezeke zaidi.

Katika kuhakikisha hilo linatokea lazima kuendelea kujenga mazingira bora ya uwekezaji na biashara. Sekta hii ikikua inakuza pia sekta nyingine kama fedha, afya na ajira na nyingine, hivyo moja kwa moja inatusaidia kufikia malengo yetu kiuchumi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents