Fahamu

Maziwa matatu yaliojificha yagunduliwa katika sayari ya Mars

Maziwa matatu ya chini ya ardhi yamegunduliwa karibu na eneo la kusini mwa sayari ya Mars. Wanasayansi pia wamethibitisha uwepo wa ziwa la nne – ambalo ishara za uwepo wake uligunduliwa 2018.

Maji ni muhimu kwa baiolojia, hivyobasi ugunduzi huo utakuwa muhimu kwa watafiti wanaotafuta uhai nje ya dunia.

Lakini maziwa hayo pia yamedaiwa kuwa na chumvi nyingi sana hali inayofanya kiumbe chochote kutoweza kuishi ndani yake.

Hali nyembemba ya hewa katika sayari ya Mars ina maana kwamba uwepo wa maji katika sakafu ya sayari huo upo chini . lakini maji yanaweza kuwepo chini ya ardhi yake.

Ugunduzi huo wa hivi karibuni ulifanyika kwa kutumia data kutoka kwa kifaa cha rada katika kituo cha angani cha bara Ulaya Esa ambacho kimekuwa kikizunguka katika sayari hiyo nyekundu tangu 2003. Mwaka 2018, watafiti walitumia data kutoka rada ya Mars ili kuripoti ishara za ziwa lenye ukubwa wa kilomita 20 ndani ya ardhi ya Mars .

Hatahivyo ugunduzi huo unatokana na tafiti 29 zilizofanywa na Marsis kati ya 2012 na 2015.

Hivi sasa kundi moja linaohusisha wanasayansi hao walioshiriki utafiti wa 2018 limechambua data kubwa zaidi kati ya rada 134 zilizokusanywa kati ya 2010 na 2019. Hatukuthibitisha ishara zilizoonekana mwaka 2018

Mars
Maziwa hayo yamezungukwa na vidimbwi vidogo vya maji

‘Hatukuthibitisha ishara zilizoonekana mwaka 2018 pekee bali pia tuligundua maeneo matatu yalio na mwanga’ , alisema mwanzilishi mwenza wa utafti huo Elena Pettinelli kutoka chu kikuu cha Roma Tre University mjini Itali.

Ziwa kubwa linazungukwa na vyanzo vidogo vya maji , lakini kwasababu ya hali ya kiufundi ya rada hiyo na umbali wake wa sakafu ya Mars , hatuwezi kubaini moja kwa moja iwapo zina uhusiano wowote.

Kundi hilo la wanasayansi lilitumia mbinu inayotumika sana katika uchunguzi wa rada kuhusu maziwa ya barafu katika eneo la Antarctica , Canada na Greenland, ikitumia mbinu hiyo kuchambua data hiyo kutoka chombo cha Marsis.

Hakuna joto la kutosha sakafuni kuyeyusha barafu , hivyobasi wanasayansi wanaamini maji hayo yana kiwango kikubwa cha chumvi. Chumvi hiyo yenye kemikali ina uwezo wa kuyafanya maji kushika barafu zaidi.

Tafiti za hivi karibuni zimeonesha kwamba maji yenye chumvi yanaweza kusalia kuwa yalivyo chini ya nyuzi joto za chini za -123C.

Maji yaliogunduliwa ktika ardhi ya sayari ya Mars
Maji yaliogunduliwa ktika ardhi ya sayari ya Mars

Iwapo Uhai unaweza kuwepo katika hali kama hiyo inategemea jinsi vidimbwi hivyo vya maji vilivyo chumvi.

Duniani viumbe vinavyojulikana kama halophiles, vinaweza kuishi katika maji yenye chumvi ya kiwango cha juu .

Dkt Orosei ambaye ndie mchunguzi mkuu alisema: Huku ikiwa uwepo wa madonge ya barafu unaweza kusababisha hali mbaya kama vile uwepo wa volkano chini ya barafu hiyo . Ugunduzi wa mfumo mzima wa maziwa unaonesha kwamba utengenezaji wake unaonekana kuwa rahisi na wa kawaida na kwamba maziwa hayo huenda yamekuwepo kwa kipindi kirefu cha historia ya sayari ya Mars.

Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana kuna uwezekano mkubwa wa uhai katika sayari hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents