HabariMichezo

Mbappe aziba kwa makusudi jina la mdhamini wa tuzo

Mchezaji wa timu ya taifa Ufaransa, Kylian Mbappe ameonekana akilificha kwa makusudi jina la mdhamini ‘Budweiser’ lililokuwa limeandikwa kwenye tuzo aliyokabidhiwa akiwa mchezaji bora wa mechi kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Qatar.

Mbappe alilificha jina hilo ambalo ni kampuni ya Bia lisionekane kwenye picha zake alizokuwa akipigwa na waandishi wa habari wakati wa kupokea tuzo hiyo kuepuka kuitangaza pombe.

Nyota huyo pia mara zote amekuwa akikataa kuhudhuria mikutano na waandishi wa habari kwa kuhofia kuulizwa maswali juu ya hatma yake ya baadae ndani ya kikosi cha Paris Saint-Germain.

Kutokana na kitendo hicho cha Mbappe kutofanya mahojiano na waandishi wa habari Shirikisho la soka nchini Ufaransa lipo tayari kumlipia faini kama adhabu kwa kitendo hicho.

Ni mashindano magumu zaidi kwa kampuni ya bia ya ‘Budweiser’ kuwahi kupitia akiwa mdhamini mkuu wa Kombe la Dunia kutokana na Qatar kuzuia uuzwaji pombe.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button