Burudani

Mbunge Babu Tale aunguruma Bungeni (Video)

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki (CCM) Hamis Taletale maarufu babu Tale amesema Serikali imewaweka watu wanaofanya kazi kama polisi kwenye Chama cha Hati Miliki (Cosota), alilodai linakwenda kuua utamaduni na muziki nchini.

https://www.instagram.com/p/CPixfqHhiVR/

Babu Tale ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 31, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka 2021/2022.
Amesema wanafahamu kuwa viongozi wa michezo wanatokana na makocha ama wachezaji, lakini kwenye Cosota viongozi hawajulikani taaluma zao.

“Lakini Cosota tumewekewa watu ambao wanakwenda kuua utamaduni na muziki wetu. Mwaka jana, Diamond Platinum na wimbo wake wa Haleluya, ulizuiwa na Cosota usipigwe. Lakini mwaka huohuo waandaaji coming to America wakaichukua kama nyimbo bora. Hapa kuna walakini kwenye Cosota,” amesema.

Akiendelea kutema nyongo bungeni, mbunge huyo amesema anazo taarifa zisizo na walakini kuwa Cosota haiwalipi wasanii  mirabaha yao licha ya vyombo vya habari kuendelea kulipa kusudi nayo iwalipe wasanii.

Tale ambaye pia ni msanii, amesema zamani alikuwa akipata fedha kutoka Kampuni ya Mmssc ya Kenya na nyingine ya Afrika Kusini, lakini kampuni hizo zilipoenda kujiunga na Cosota, sasa wasanii hawalipwi tena.

Amemtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa ajibu hoja yake ya wasanii wanaoidai Cosota watalipwa lini na asipofanya hivyo, atashikilia shilingi kwenye mshahara wa waziri huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents