HabariSiasa

Mbunge Cherehani ahoji kuhusu wafugaji walioshinda kesi

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Peter Cherehani siku ya leo bungeni katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amehoji juu ya kauli ya Serikali kuhusu malalamiko ya wafungaji waliotaifishwa na kuuziwa mifugo yao katika hifadhi za taifa kisha kushinda kesi Mahakamani.

Akijibu swali hilo Bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa maeneo yote yaliyotolewa amri ya mahakama kutekeleza amri hiyo kwani kufanya hivyo kutajenga mshikamano baina ya mihimili ya serikali na kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake kupitia chombo husika kinachosimamia haki ambacho ni mahakama.

Waziri Mkuu amesema “Natambua kuwepo kwa migogoro mingi kati ya wafugaji na wakulima, wafugaji na maeneo ya hifadhi, na kwakuwa jambo hili ni la kisheria sana na lina sheria zake pale ambapo imeamriwa ni lazima tutekeleze kwasababu hakuna anayeweza kupinga amri ya mahakama”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents