Mbunge mwenye ugonjwa wa vitiligo afedheheshwa bungeni (+ Video)

Spika wa bunge la Mauritius amekosolewa vikali kwa kumuaibisha mbunge mwenye ugonjwa w angozi wa vitiligo, hali ambayo husababisha sehemu ya ngozi kuwa nyeupe zaidi.

“Angalia uso wako!” Spika Sooroojdev Phokeer alipaza sauti akimwambia mbunge Rajesh Bhagwan mara 11.

Hii ilifuatia matamshi ambapo mbunge alimuelezea spika kama “mlevi” na “aibu” Video ya malumbano hayo imeshirikishwa umma kwenye mtandao waTwitter:

Vitiligo ni ugonjwa unaosababisha mtu kupoteza sehemu ya ngozi yake ya kawaida au rangi yake. Kauli hizo zimeibua miito ya kumtaka spika ajiuzulu na zimelaaniwa kote nchini na nje ya nchi.

Baada ya malumbano hayo Bw Bhagwan alisema ilikuwa ni “jambo la aibu ” kuzungumzia kuhusu afya ya mtu, akisema spika ni”fedheha kwa taifa”. Katika ujumbe wake wa Twitter kikundi cha Uingereza kinachounga mkono Vitiligo kiliita kauli ya spika “fedheha”.

“Vitiligo sio maelezo ya tabia yetu,” kilisema kikundi hicho, kikiongeza kuwa uso wa Bw Phokeer’ haupaswi “kuonesha aibu” kwa ” kumfedhehesha na kutomheshimu”.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CSLu5mpjble/

Related Articles

Back to top button